Makasisi wafungwa miaka 40 kwa kuwanyanyasa watoto

Mahakama nchini Argentina imewahukumu makasisi wawili wa Kanisa Katoliki la Roma kifungo cha zaidi ya miaka 40 jela kila mmoja v kwa kuwanyanyasa kingono watoto viziwi katika shule ya kanisa.

Horacio Corbacho na Nicola Corradi, pamoja na muhudumu wa bustani, walipatikana na hatia ya kuwabaka na unyanyasaji katika shule ya kikatoliki iliyopo katika jimbo la Mendoza kuanzia mwaka 2004 hadi 2016.

Waathiriwa kadhaa walikuwa mahakamani kushuhudia kutolewa kwa hukumu Jumatatu.

Kesi hiyo imeishitua Argentina, nchi ambayo anatoka Papa Francis, huku wengi wakilishutumu kanisa kwa kuzorota kuchukua hatua.

Kanisa Katoliki limekabiliwa na shutuma za unyanyasaji wa kingono wa watoto katka maeneo mbali bali duniani katka kipindi cha miongo michache iliyopita.

Mahakama ilibaini nini?

Jumatatu, mahakama katika mji wa Mendoza alimhukumu kasisi wa Kiargentina kifungo cha miaka 45 jela.

Padre huyo mwenye umri wa miaka 59 alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto katika shule inayofahamika kama Instituto Antonio Provolo de Mendoza katika mji wa Luján de Cuyo.

Corradi, mwenye umri wa miaka 83-mwenye uraia wa Italia, alihukumiwa kifungo cha miaka 42 jela.

Alikuwa anachunguzwa kwa unyanyasaji alioutekeleza katika shule ya Verona, nchini italia miaka ya 1970, lakini hakuwahi kushitakiwa.

Armando Gómez, muhudumu wa bustani katika shule ya Luján de Cuyo alihukumiwa kifungo cha miaka 18 jela.

Hawawezi kukata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama kwa mujibu wa sheria za Argentina kuhusu makosa hayo.

Soma mengi