Sikufutwa kazi na K24, Mwanaisha Chidzunga aeleza dili mpya

Screenshot_from_2019_12_03_16_04_11__1575378286_28624
Screenshot_from_2019_12_03_16_04_11__1575378286_28624
Aliyekuwa msomaji habari katika runinga ya K24 Mwanaisha Chidzunga amekana taarifa kuwa alipigwa kalamu katika kampuni ya Media Max.

Media max ni kampuni na ambayo inamiliki runinga ya K24 na baadhi ya maredio hapa nchini.

Kampuni hii iligongwa vichwa vya habari muda mchache uliopita kwa kuwaachisha kazi wafanyakazi wake.

Akijitetea kutokana na swala la kufutwa kazi, mwanadada huyu amesema kuwa mkataba wake ulikuwa umemalizika kabla ya kampuni hiyo kutoa tangazo la kuwafuta wafanyakazi wake.

Kwa sasa Mwanaisha amejiunga na biashara zake.

"Mkataba wangu ulimalizika tarehe 1 Novemba na hiyo ni miaka minne kutoka 2015. Nilikuwa na ruksa ya kusajili mkataba huo upya ila nilikuwa nishafanya uamuzi wa kutofanya hivyo..."

"Kwangu mimi lazima maisha yaendelee. Kuna maisha mengine zaidi ya kuonekana katika runinga. Namaanisha kuna utandawazi, mtandao wa YouTube na kadhalika..."

"Mimi huwa tayari muda wowote. Mlango mmoja ukifungika mwingine unafunguka. Mimi huwa tayari kwa nafasi yoyote inayojiri. Sio big deal. Mwaka ujao 2020 utakuwa wa mafaniko..."

Mwanaisha alifunguka haya yote katika hafla ya tuzo za Kalasha.\

Katika tamasha hizi, mwanadada huyu alikuwa anagombea kitengo cha muigizaji bora katika tasnia yua filamu.

Aidha, mipango ya kuanzisha kipindi katika mtandao wa You Tube upo,

Nitakwenda kuanzisha YouTube channel yangu bkwa jina Dada Uncensored. Lengo litakuwa kuhusu kuhamahamsisha wamama, kuwamotisha pamoja na mawaidha ya kutengeza nafasi za biashara na ajira.