'Alinilazimisha kulamba uume wake, akanibaka na kuiba pesa zangu," asimulia kortini

Mbusiro
Mbusiro
Mwanaume ameshtakiwa kwa kosa la kumshambulia mhudumu wa kike wa mkahawa kwa kisu, akamlazimisha kulamba uume wake, akambaka na kisha kumwibia shilingi 630 kutoka akaunti yake ya M-Pesa.

Charles Mbusiro hata hivyo alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkaazi wa Kibera Boaz Ombewa.

Mbusiro anadaiwa kumnajisi kidosho huyo baada ya kumlazimisha kumvuta hadi kichakani katika eneo la Uthiru jijini Nairobi Disemba 4.

Aidha, alishtakiwa kwa kumshika sehemu za siri za Angela (silo jina lake rasmi) na kumwibia shilingi 130 kutoka begi lake na shilingi 600 kutoka akaunti ya M-Pesa.

Ripoti ya polisi inasema kuwa Mbusiro alimshambulia mwanamke huyo alipokuwa akitoka kazini.

"Nilitoka kazini Githurai ninapofanya kama mhudumu wa mkahawa na nilipofika Uthiru nilinunua chapati na mayai na kisha kutembea kuelekea kwangu. Kulikuwa na mwanaume wa umri wa makamo mbele yangu," ripoti ya polisi inasema.

Anasema kuwa Mbusiro alimtishia kwa kisu na akalazimika kukubali amri zake bila hiari ili kunurusu maisha yake.

"Alinishika kutoka nyuma nilipogeuka kumwaangalia. Alinitishia kwa kisu huku akisema nikubali au aniue," alisema.

Kisha jamaa huyo alimpeleka kwenye msitu na kumnajisi na kumwibia.

"Alinivuta hadi kichakani chenye mahindi na nyasi nyingi, akanilazima nilambe uume wake na kunibaka mara kadhaa kisha akaiba pesa zangu," alisema.

Kidosho huyo anasema kuwa alilazimishwa kuvua nguo zake na kuweka juu ya mti wa parachichi.

Baada ya kumaliza haja yake, msichana huyo alilazimishwa kujipangusa kwa nguo zake na kutishia kutotoa siri hiyo kwa mtu yeyote.

"Alinilazimisha kutoa pin yangu ya mpesa na kujitumia pesa zote kisha akatoa simcard yangu," alisema.

Mbusiro alikana mashtaka hayo na kupewa bondi ya shilingi 600,000 na mdhamani wa kiasi hicho.

Kesi hiyo itasikizwa tena Machi 3 mwaka ujao.