(+Picha) Mchumba wa mcheshi Dr Ofweneke aonyesha ujauzito wake

Screenshot_from_2019_12_12_11_34_07__1576139700_63158
Screenshot_from_2019_12_12_11_34_07__1576139700_63158
Mpenzi wa mcheshi maarufu Dr Ofweneke amefunguka kuwa ana ujauzito na ana hamu kubwa sana ya kupata mtoto hivi karibuni.

Kando na kuwa mcheshi ,Ofweneke anaendesha kipindi katika runinga.

Ofweneke pia anafahamika kama Sande Bush na ni miongoni mwa mastaa wakubwa katika tasnia ya ucheshi na uanahabari hapa nchini.

Mpenzi wake wa sasa ni Christine Tenderness.

Sande alipatana na mchumba huyu baada ya kutemana na Niccah The Queen.

Kwa sasa miaka mitatu imeisha tangu walipoachana.

Kuna ishara kuwa huenda Ofweneke ameamua kutulia katika ndoa na mrembo Christine.

Kupitia mtandao wa Insta, Christine alichapisha picha za ujauzito.

Tazama baadhi ya picha hizo: