Katika mitandao ya kijamii, wakili huyu ambaye ana uraia tata amesema kuwa haogopi kusafiri nchini tarehe 11, Januari 2020.
Aidha, Miguna amechapisha nambari za dharura za kupiga iwapo kutatokea kizungumkuti katika safari yake.
https://twitter.com/MigunaMiguna/status/1206421286970445824
Miguna alikuwa mgombezi wa nafasi ya ugavana kaunti ya Nairobi katika uchaguzi uliopita.
Wakili huyu alifurushwa nchini mwaka jana baada ya tukio la kuapisha kinara wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga.
"Ndege nitakayosafiria itatua uwanja wa JKIA tarehe 11,Januari 2020..." Ametangaza Miguna.
https://twitter.com/MigunaMiguna/status/1206230998104649729
"Hatutaita watu kuandamana. Huo utakua ujinga. Kihistoria, mageuzi na maendeleo ya kusonga mbele katika jamii husababishwa na thuluthi tatu ya watu. Kama hautaki mageuzi, tulia nyumbani. Wazalendo milioni 1 wataandaamana..." Alisema Miguna.