Kulingana na matokeo hayo Mabingwa Barca watasalia kileleni mwa La Liga na alama 36 sawia na Madrid ambao wamefunga magoli chache. Hii ilikua mara ya kwanza pande hizo mbiil zimetoka sare tasa kwa miaka 17.
Manchester City itapambana na mahasidi Manchester United katika nusu fainali ya kombe la carabao, baada ya pande zote mbili kufuzu jana.
City iliilinyuka timu ya daraja la kwanza Oxford United 3-1 huku Raheem Sterling akifunga magoli mawili, nao United waliwanyuka timu ya daraja ya pili Colchester United 3-0.
Anthony Marcial na Marcus Rashford wakifunga magoli hayo kabla ya Ryan Jackson kujifunga mwenyewe. Leicester City ambao waliwanyuka Everton 4-2 kupitia penalti baada ya sare ya 2-2 , watapambana na Aston Villa ambao waliwalaza Liverpool 5-0 siku ya Jumanne.
Mchezaji wa akiba Roberto Firmino alifungia Liverpool goli la dakika ya 91 dhidi ya Monterrey na kuisadia klabu yake kufuzu kwa fainali ya kombe la klabu bingwa duniani, mjini Doha Qatar kwa ushindi wa 2-1.
Vijana wa Mexico walikua wameswazisha kupitia Rogelio Mori katika kipindi cha kwanza baada ya Naby Keita kufungia the Reds goli la ufunguzi. Liverpool sasa watapambana na Flamengo ya Brazil ambao walilaza Al Hilal ya Saudi Arabia's mabao 3-1 katika fainali ya Jumamosi.
Nchini Italia Juventus walirejea kileleni mwa ligi ya serie A kutokana na ushindi wa 2-1 dhidi ya Sampdoria huku Paulo Dybala na Cristiano Ronaldo wakifungaia Juve magoil yao katika kipindi cha kwanza.
Mlinda lango mkongwe Gianluigi Buffon mwenye umri wa miaka 41 alifikia rekodi ya Paolo Maldini ya kucheza mechi mia sita arubaini na saba Serie A. Juve sasa wana alama 42 tatu mbele ya Inter Milan wanaoshikilia nafasi ya pili wakiwa na mechi moja mkononi.