Je ni kipi kikuu chaweza fanyika iwapo Miguna atarejea nchini?

Mara ya mwisho kuskia kuhusu kukuru kakara za Miguna ni wakati wakili wake John Khaminwa alipowasilisha kesi kortini akitaka ilani iliyotolewa dhidi ya mteja wake asiruhusiwe kuja nchini Kenya iondolewe.

Mapema mwezi huu, Miguna alizuiwa mara mbili kuabiri ndege ya kuja Kenya baada ya ilani kutolewa dhidi yake ili aisruhisiwe kuingia nchini.

Serikali hata hivyo inashikilia kwamba haijatoa agizo kama hilo na kumekuwa na mvutano kuhusu hatma ya ziara ya wakili huyo mtatanishi.

Hata hivyo swali tunalojiuliza ni je, iwapo Miguna huenda akaruhusiwa kuja nchini, ni kipi kikuu ambacho anaweza kufanya?

Tumeorodhesha baadhi ya vitu au mambo yanayoweza fanyika;

Kumpiga Raila Vita

Hivi sasa, wakenya wengi wanmsifia Raila Odinga kwa jinsi alivyo ungana na rais Kenyatta ili kudumisha umoja na amani nchini. Shughuli ya 'handshake' ilifurahiwa kwani ilimaliza migogoro kati ya serikali na upinzani.

Kabla ya kufurushwa kwake, Miguna alikuwa miongoni mwa marafiki wa ngazi ya juu wa Raila lakini hilo lilibadilika alipofika Canada. Miguna amekuwa akimshambulia Raila pamoja na viongozi wengi nchini akimuita msaliti wa wakenya.

Hilo basi laweza endelea huku Miguna akifanya mikutano nchini kote.

Kuandika kitabu kingine

Miaka kadhaa iliyopita, Miguna ambaye aliwahi fanya kazi kwa karibu na Raila Odinga, aliandika na kuzindua kitabu kwa jina Peeling Back the Mask: A Quest for Justice in Kenya.

Katika kitabu hiki Miguna anazungumzia uhusiano wake na Raila Odinga huku akifichua jinsi urafiki baina yao uliisha, miongoni mwa mambo mengine ya kisiasa nchini.

Basi iwapo Miguna anaweza ruhusiwa kurudi nchini, sioni ni kipi kitamzuia wakili huyo kuandika kitabu kinachoangazia masaibu aliyopitia baada ya uchaguzi wa 2017.

Kujiunga na Ruto 

Jinsi siku zinavyopita, ndivyo tunaona urafiki na undugu baina ya Uhuru Kenyatta na naibu wa rais WIlliam Ruto ukididimia. Hivi sasa, Raila Odinga na Uhuru Kenyatta wanazungumza lugha moja kinyume na Ruto na wandani wake wanaokashifu muungano wao.

Hili pia laweza pelekea kuvunjika kwa chama cha Jubilee ifikapo mwaka wa 2022 iwapo Uhuru hatomuunga Ruto mkoono katika uchaguzi.

Ruto na Miguna wana jambo moja sawia, damu zao na damu ya Raila Odinga hazipatani na hilo laweza wafanya wawili hao marafiki dhidi ya 'adui' wao.

Basi usishangae Ruto akanufaika kumsuka na kumfanya mmoja wa wandani wake ili aweze kupigana na Raila ifikapo 2022.

Kuwania kiti 

Kenya twajua vyema kuwa wanasiasa wengi walibahatika kufika walipo kufuatia umaarufu fulani, wengine walikuwa wanahabari, wengine walipata umaarufu kufuatia mabishi dhidi ya wanasiasa na kadhalika.

Basi kwa upande wake Miguna, migogoro dhidi ya serikali imempa umaarufu wa kutosha na iwapo ataamua kuwania kiti chochote humu nchini, kando na kiti cha Ugavana wa Nairobi, basi hatokuwa na wakati mgumu kuuza sera zake.