Ilikuaje: Najuta sikumpa mtoto wangu malezi bora -Mary Njeri

Katika kitengo cha ilikuaje na mtangazaji wetu Massawe Japanni, tuliweza kuwa na mgeni ambaye anafahamika kama Mary Njeri aliyewapoteza watoto wake wawili kwa njia tofauti.

"kifungua mimba aliuwawa 18 machi 2012 na polisi kwa sababu alikua muhalifu, na wa pili aliweza kuuwawa na rafiki yake septemba 2013,

 Ibrahim Njoroge ambaye alikuwa kifungua mimba aliuwawa nikiwa nipikia dada yangu mboga kwa sababu alikuwa na sherehe ya siku ya kuzaliwa  ya mtoto wake," Alieleza Mary.

Mary alieleza kwa uchungu na kulia kwa uchungu ambao aliweza kupitia baada ya kuambiwa kuwa aliyeuwawa na polisi alikuwa mwendazake Njoroge.

"Tulisikia risasi tukiwa kwa nyumba kisha nikaambia dadangu aweze kuenda na kuangalia ni nini kilichokuwa kinaendelea,

"Alikaa sana na kisha aliporudi nikaambiwa ni kijana wangu ambaye ameuawa," Mary Alisimulia.

Njeri alisema kuwa hakuwa na wakati na watoto wake kwa sababu alikuwa ameshikana ili kuwatafutia watoto wake riziki.

Mary alieleza zaidi na kusema kuwa alitengana na mume wake mwaka wa 1995 kwa sababu mumewe alikuwa na wanawake wengi.

"Nilitengana na baba wa watoto wangu kwa sababu alikuwa ameshiriki ngono na binamu yangu," Mary alieza.

Mtoto wake wa pili aliuwawa na rafiki yake kwa njia tatanishi isiyo julikana na hadi kufikia sasa hajawahi jua sababu ya rafiki yake aliweza kuchukua uhai wa mtoto wake.

"Mtoto wa pili alipigwa risasi na rafiki yake, aliyemuua alinipigia simu na kunifahamisha kuwa kijana wangu alikuwa ameuliwa,

"Baada ya mazishi kijana ambaye alinipigia simu ndiye nilijua kuwa ni yeye alikuwa amememuua, kijana huyo alikuwa amempachika msichana wa miaka 16 mimba.

"Wote walikuwa watoto wa shule, mtoto wangu alikuwa anaelekea kidato cha nne kisha nikaamua kuchukua majukumu ya kulea mtoto huyo," Alizungumza Mary.

Mary alisema kuwa kijana huyo wa pili alikuwa amesema kuwa aliweza kutoroka shuleni baada ya kitendo hicho na kuenda kuishi na rafiki yake.

"Niliongea na yeye na akarudi nyumbani, wakati alipokua anarudi nyumbani alipigiwa simu na rafiki yake na kumwambia wapatane hapo ndipo aliweza kupata nafasi ya kuumua." Njeri Alisema.

Mwanamke huyo alieleza kuwa hadi sasa hajawahi pea mtoto wake haki ambaye aliuwawa na rafiki yake kwa sababu alijua jambo hilo litamuumiza moyo.