Kaunti ya Kiambu sasa ina gavana mpya baada ya James Nyoro kuapishwa leo ili kuichukua nafasi ya Ferdidand Waititu ambaye bunge la senate lilipitisha hoja ya kumwondoa afisini siku ya jumatano .Katika hafla ya kufana iliyoandaliwa kwenye makao makuu ya kaunti hiyo Nyoro alikula kiapo cha kuchukua wadhfa huo huku akishangiliwa na wafuasi wake .
Nyoro sasa ni gavana wa tatu kuhudumu katika kaunti hiyo chini ya katiba mpya . Usalama uliimarishwa katika makao makuu ya kaunti hiyo kabla ya hafla ya kumuapisha Nyoro kuanza . wageni walioalikwa walikuwa wameketi katika jukwa la hafla kufikia saa sita mchana .
Kwingineko juhudi za gavana wa zamani Ferdinand Waititu kuzuia kuandaliwa kwa hafla ya kumuapisha Nyoro zilitumbukia baada ya mahakama kuu kukataa kuzuia shughuli hiyo . Jaji Weldon Korir ameshikilia kwamba pande zote zinafaa kufika mbele ya jaji James Makau siku ya jumatatu kwa kikao cha kusikiliza mawasilisho kutoka pande zote .