Mtangazaji wa runinga Betty Kyallo ameonyesha ghadhabu yake na mtindo wa mayaya wa nyumbani kufanya wizi majumbani walikoajiriwa licha yaw engine kulipwa vizuri .Mtangazjai huyo wa habari wa K24 Alionekana kuhamakishwa na tabia hiyo na kuyapeleka manung’uniko yake katika ukurasa wake wa instagram .
Kyallo alikuwa akilalama kwamba badahi ya ‘maids’ bado wana tabia mbaya ya kuwaibia waajiri wao licha ya kuwa wanalipwa hata shilingi elfu 18 kwa mwezi!.
Haijabainika iwapo Betty amekuwa mwathiriwa wa tabia hiyo mbaya ya wafanyikazi wa nyumbani lakini uchungu wake unaweza kueleweka na waliowahi kuathiriwa na ukatili unaofanywa na wafanyikazi kama hao. Kyallo amewarai wazazi kupitia ujumbe wake wawe waangalifu kuhusiana na wafanyikazi wa nyumbani na kutowaamini kwa asilimia 100 na kila jambo nyumbani .