Nakukosa sana: Vanessa aandikia bintiye Gianna ujumbe

Baada ya ajali ya helkopta iliyosababisha kifo cha nyota wa basketiboli Kobe Byrant na bintiye Gianna mkewe Kobe amekua akiandika jumbe za kumkosa bintiye na mumewe.

Ajali hiyo ilitokea mwezi jana na kumuacha Vanessa katika majonzi kwa kuwapoteza watu wa karibu na moyo wake. Aliweka picha ya bintiye katika mtandao wa kijamii, baluni na jezi ya Gianna.

"Gianna, nakukosa sana, nimekua mwenye bahati nzuri kwa kuamka kila asubuhi na kuona sura yako yenye tabasamu kwa miaka kumi na tatu.

Natamani ingekua hivyo hadi mwisho wa kupumua kwangu, nakupenda sana #2 #MAMBACITA #GIGIBRYANT ❤️." Ujumbe ulisoma.

Vanessa alimsifu Gianna katika ujumbe huo.

"Gigi nakupenda sana nakupeza mwanangu, ulitufunza ukitenda wema hata kama ni jambo ndogo kwa hakika si dogo bali unapaswa kutenda wema kwa roho moja.

Mama atazidi kukupenda na kukukosa  MAMACITA. ❤️#2 🏀." Aliandika.

Mkewe Kobe hakumsahau mumewe alimuandikia ujumbe pia katika mtandao na kumwambia kuwa alikua rafiki wa dhati.

Vanessa ambaye ana miaka,37, alikuwa katika ndoa na  mwenda zake Kobe kwa takribani miaka ishirini huku akiweka picha yake akiwa ametabasamu na kuandika ujumbe chini ya picha hiyo.

"Rafiki yangu wa dhati, baba wa watoto wangu na kupeza sana pia,mcheshi na kupeza kwa usemi wako wa  “BONJOURNO PRINCIPESSA/REINA”. Vanessa Aliandika.