zinakaa vitenge! Wakenya wazungumzia sare mpya za wanariadha

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii hawajafurahishwa na sare mpya za wanariadha zilizozinduliwa na kampuni ya marekani ya Nike.

Nike walizindua sare za nchi kadhaa ikiwemo Kenya miezi kadhaa kabla ya michuano ya Olimpiki itakayo andaliwa mjini Tokyo, Japan.

Hata hivyo, wakenya walikimbilia mitandao ya kijamii wakisema kuwa sare zetu sio za hali ya juu au hazivutii macho ikilinganishwa na sare za Nigeria, marekani na nchi zingine ambazo zimefuzu Olimpiki.

Isitoshe, wengine walizilinganisha na nguo za aina ya vitengo huku wakionesha kugadhabishwa kwao.

Soma baadhi ya jumbe zao,

Kimutai: Ours is a raw deal from Nike. By the way, I can go to court because there was no public participation. Our athletes cannot compete with hexagonal honey combs patterns. We need national colours of red, black green and with in patter of shield and spear. Period.

Kenwes: Mlitengenezewa githurai hii ama?

Childmarakwet: Ushenzi sana,who thought about it? KENYANS ARE MORE CREATIVE THAN THIS. Tragic.

Counting days: It can't be too late to get another sponsor who has taste?

Mimi ndimi: Wacheni mchezo aki..hata kama ni nguo za michezo!!!

Tizama picha zifuatazo: