Safiri salama,' Vijana wa rais mstaafu hayati Moi wasoma historia yake

unnamed(7)
unnamed(7)
Ibaada ya wafu ya rais mstaafu hayati Daniel Arap Moi, imefanyika  katika uwanja wa Nyayo mamillioni ya wakenya na viongozi kutoka mataifa tofauti wakijitokeza ili kumpa heshima ya mwisho mzee Moi.

Waliosoma historia  yake ni vijana wake  huku wakiwa wamejawa na hisia na kulingana na historia hiyo Moi alibarikiwa watoto wanane watano wavulana na watatu wasichana .

Kifungua mimba akiwa Jenniffer Chemutai , mtoto wa pili akiwa  mwendazake Jonathan Toroitich aliyefariki mwaka wa uliopita, John Mark, mbunge wa Rongai, Raymond, baada yake Moi alibarikiwa na mapacha wawili, Philip na Doris,na Gideon akiwa kitinda mimba wa familia ya Moi.

Mwanawe Philip alifungua ibada hiyo na neno la Mungu kutoka katika kitabu cha ufunuo 14:13.

"Kisha, nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema, “Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata.”

Raymond Moi alisoma historia ya babake kuanzia siku aliyozaliwa hadi siku ya jua kutua juu ya maisha yake.

Raymond  aliendelea kusoma historia ya mzee Moi na hata akaingiza utani kwa wakati mwingine haswa alipotaja wanawe mwendazake na kusema kuwa pia yeye alikuwa miongoni mwa wale watoto,ukumbi ukapasua kicheko.
Moi aliaga dunia Jumanne ya tarehe 7 Februari mwaka huu, saa 5:20 asubuhu, mnamo tarehe 12/02/2020 mwendazake atazikwa maeneo ya Kabarak nyumbani kwake kaunti ya Nakuru.
Kabla ya kuzikwa kutakuwa na ibada yake katika chuo kikuu cha Kabarak.