Sababu za Sonko kuzuiwa kuingia katika eneo la wageni waheshimiwa, Kabarak

Gavana wa Nairobi, Mike Sonko alijipata katika hali ya aibu alipozuiwa kuingia katika eneo lililotengewa wageni waheshimiwa huko Kabarak, huku mazishi ya mzee Moi yakiendelea.

Sonko na aliyekuwa waziri mkuu, Raila Odinga, walifika dakika chache baada ya rais Kenyatta kuwasili katika chuo kikuu cha Kabarak. Hata hivyo, Raila hakuzuiwa kuingia ila tu Sonko.

Kama ilivyo mtindo, iwapo rais anahudhuria hafla yoyote, wananchi na viongozi wanapaswa kuwasili mapema na kuketi kabla kuwasili kwake.

Hata hivyo, baada ya mda mchache alikubalishwa kuingia kwenye hema.