Ilikuaje: Mume wangu aliambia wakwe wangu nataka kumuua-Mary Princess

IMG_0346(1)
IMG_0346(1)
Katika kitengo cha ilikuaje Mary Princess alisimulia jinsi walitafuta mali na pesa na mumewe lakini baadaye akaja kumsaliti na mumewe kuenda na mali zote na kumuachia watoto bila chochote.

Mary alikaa katika uhusiano huo kwa miaka kumi.

"Tulitafuta mali na mume wangu lakini baadaye akanisaliti na mwanamke mwingine na kuenda na mali yote, kwa hakika ni mimi nilikuja na mawazo yote ya kutafuta mali hiyo

Nilijua mumu wangu anauhusiano wa nje baada ya kumnunulia mwanamke huyo gari kisha mwanamke huyo akanitumia picha ya gari hilo na makartasi yameandikwa jina lake." Alieleza.

Baada ya mume wake kumtoroka Mary alirudisha nyumba kwa benki ili kulipa mkopo wao, nyumba hiyo ilikuwa ya millioni,13.

"Mume wangu alishauriwa na marafiki ambao alidhani ni wazuri na kumshauri aoe bibi wa pili kwa sababu alukuwa na pesa za kuwakimu wanawake wawili." Alizungumza Mary.

Mary alisema ashaamsameha mume wake kitambo kwa kitendo hicho alichokifanya.

"Nilimsamehe baada ya miezi mitatu, mnamo mwaka wa 2018 alinipigia simu na kuniambia hana chochote na hata hajakula chochote kwa siku tatu

Nilimtumia mia tano na tangu wakati huo hatujawahi zungumza tena." Mary Aliongea.

Wakati mume wake alikuwa anataka kumtoroka Mary alimzingizia kuwa anataka kumuua.

"Mume wangu aliwaambia wakwe wangu kuwa nataka kumuua, hiyo ilikuwa sababu tosha ili atoke kwangu, baadaye walikuja kujua ukweli na tunamawasiliano mema wakati huu." Alisema.