Penzi gushi;mwanaume asumulia jinsi alivyo achwa na mpenziwe siku ya wapendanao

hqdefault
hqdefault
Tarehe 14/02 ya kila mwaka wapenzi huwa wanaingoja sana kwa sababu imetengwa kwa ajili yao,japo kwa Simon kitumbua kilitifuka na hakuadhimisha siku hiyo vile alivyokuwa anadhania.

Kupitia mtandao wa kijamii mwanaume Simon alisimulia jinsi alivyoachwa na mpenzi wake siku ya wapendanao, akiandika uumbe alisema,

"mwaka jana nilikuwa nataka kuenda katika onyesho la churchill na sikuwa nataka mpenzi wangu ajue, kwa sababu sikuwa na hela ya kutosha,

Nilikuwa tu na elfu mbili za kujivinjari na marafiki na kulipa tikiti ya kuingia kwa onyesho." Aliandika Simon.

Ilimbidi amdanganye mpenzi wake yupo kazini ili aende tu pekeyake.

"Nilimpigia mpenzi wangu simu nikamwambia kuwa mwajiri wangu ametutuma kazini mjini Mombasa kwa hivyo asijali tutasherehekea wikendi,

Alinijibu akaniambia ni sawa pia yeye hasikii vizuri atashinda kwa nyumba akiwa amelala." Alieleza.

Kwa kweli waswahili hawakukosea waliposema siku za mwizi ni arobaini, hakuna yeyote alikuwa anasema ukweli kati ya hao wawili.

"Nilipofika katika onyesho nilitupa macho mbele nikamuona mpenzi wangu na mwanaume mwingine, nilimtumia ujumbe nikamwambia nimefika Mombasa na anaendelea aje

Aliniambia anapika ndio ale apumzike, kwasababu nilikuwa nimemwambia nimeenda Mombasa singedhubutu kuenda alipokuwa

Bali na hayo mwanaume huyo alikuwa na walinzi ambao walikuwa wanaogofya sana." Alisema.

Kwa kweli huwezi kaa chini wala kulaza damu unapoona kipenzi chako na mwanaume au mwanamke mwingine alisimulia masaibu yake yaliyomsibu.

"Nilimpigia simu hakupokea alinitumia ujumbe na kuniambia kuwa amemaliza kupika na anaenda kuoga kwa hivyo tutaongea baadaye

Nilishindwa mtu anaenda kuoga na yupo kwenye onyesho la churchill." Alisimulia Simon.

Vituko vyao vilianza wakati alipoona mpenzi wake na mwanaume huyo penzi lao likiwa limenoga sana.

"Niliona wameanza kupeana busu nilichukua simu kwa haraka na kumtumia ujumbe nikamwambia niko katika onyesho la Churchill

Nilimuelekeza nilipokuwa nimekaa na kuniangalia, zile za huyu si alikuwa Mombasa anafanya nini hapa nami namwangalia huyu sini mgonjwa anafanya nini hapa. Simon Alieleza.

Vituko vyao vilifika kilele baada ya onyesho hilo kuisha.

"Onyesho ilipoisha nilimfuata alipokuwa anaenda na jidume huyo, walipofika kwenye gari nilifika upesi nikaongelesha kipenzi changu na kumuuliza

Yaani babe unaenda 'kunyanduliwa' na jidume hili alifunga kioo na hakujibu chochote hivo ndivyo alienda." Alisimulia.