Nililala nikaamka na lafudhi ya Marekani - Mwanadada kutoka Uganda asema

Mwanadada mmoja kutoka nchi jirani ya Uganda ambaye anaiga wamarekani anapozungumza, amewashtua wengi baada ya kudai kuwa sio kupenda kwake ila aliamka siku moja na kujipata na lafudhi hiyo.

Kwa wale wasiojua maana ya neno lafudhi ni; Lafudhi ni namna ya pekee ya kutamka lugha kutokana na lugha ya mwanzo/awali ya mzungumzaji au eneo alipojifunza lugha.

Akizungumza na runinga ya Urban TV, mwanadada huyo ambaye ni mwanabiashara kwa jina Victoria Akao, alisema kuwa lafudhi yake ni kama zawadi kutoka kwa maulana na kwa kweli hajawahi tembelea nchi ya Marekani.

“God does extraordinary stuff, right? So I just woke up one morning and the accent just came on and I was like ‘okay’ and people started saying ‘Hey what’s up with it?’ And I was like ‘I don’t know!’ because I did not even realise I was speaking like this, so its God,” Victoria alisema.

Mwanadada huyu amenikumbusha slay queens wetu humu nchini ambao hujipatia lafufhi feki kila wanapowaona wazungu kwa minajili ya kuwavutia.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na mungu wake, Victoria alisema kuwa ameokoka.

Tizama kanda ifuatato na utueleze iwapo Victoria anajifanya ama ni ukweli lafudhi yake ni kipawa kutoka kwa mwenyezi mungu.

Tazama kanda hii