Majuto: ‘Nilitoa mimba ya miezi sita kwa sababu mpenzi wangu alikuwa hanipi pesa’

pregnant
pregnant
Kupata mtoto  ni Baraka.  Lakini kuna akina dada mabo wametekeleza mauaji kwa kuavya mimba bila kujua matokeo na kasha baadaye kujutia .

Ingawaje kuna hali zinazokubalika kwa mwanamke kuruhusiwa kuavya mimba ,sababu nyingi ambazo akina dada  hutoa mimba  hazikubaliki na ni ukatili mkubwa .Iwpao maisha ya mama yapo hatarini na kwa ushauri wa daktari basi inaruhusiwa mimba ile kutolewa ili kuyaokoa maisha ya mama .  Aliyofanya  Millicent Weru* yamemrudi na anajutia kwa sababu  aliitoa mimba ya miezi sita ili kumuadhbu mpenzi wake ambaye anasema aolikuwa ‘mchoyo’ na hakuwa akimpa pesa kwa hivyo aliogopa kwamba hangeweza kumsaidia endapo angejifungua  mtoto yule. Baada ya uhusiano wa miaka mitatu , Millicent na mpenzi wake  Eric waligundua kwamba   walikuwa wazazi watarajiwa . Hawakuwa tayari kuanza kufanya ulezi lakini Eric alimhakikishia Millicent kwamba angemtunza pamoja na mtoto wao ambaye hakuwa amezaliwa .  Mambo yalikuwa mazuri  hadi wakati  Mimba hiyo ilikuwa imetumu miezi sita –miezi mitatu kabla ya kujifungua wakati Millicent na Eric  walipogombana na kurushiana maneno makali .

Kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao walikuwa wametofautiana vikali sana na hali haikurahisishwa na uja uzito wa Millicent. Alikuwa akidai kwamba kwa muda sasa Eric alikuwa  ameanza kuwa mgumu kutoa pesa za kumsaidia  na alihofia huenda hilo likaendelea hata wakati atakapojifungua  na angekosa kumtunza mtoto wao . Eric alijaribu kueleza kwamba hali kiuchumi kwake ilikuwa mbaya na wakati mwingi hakuwa na pesa za kumpa Millicent ambaye alikuwa bado anaishi kwao . Milly kwa upande wake alikuwa  na  wazo kwamba Eric alikuwa keshapata mpenzi wa pembeni na hivyo alikuwa amemtelekeza mIlly ambaye alikuwa na uja uzito .Pia alikuwa akidai kwamba huenda Eric alikuwa akimuangazia sana mpenzi wake mpya na kumpa pesa badala ya kumtunza yeye na  mtoto wao  ambaye alikuwa njiani .

Alipozungumza na baadhi ya rafiki zake kuhusu hofu hizo walimshauri  aitoe mimba hiyo . Licha ta kuwepo hatari ya kuitoa mimba ya miezi  sita ,Milly alikuwa ameshakata kauli ya kuavya mimba na safari yake ya majuto ikaanza . Alishauriwa kwenda katika hospitali moja Kangemi ambako wanawake wasotaka kujifungua walikuwa wakipewa tembe ya kuavya mimba . Hospitalini ,hakuwa na fedha za kutosha ili kupewa dawa na pia kulazwa ili utaratibu mzima wa kuiondoa mimba ile ufanywe na kukamilishwa . Ombi lake kwamba asaidiwe na angeleta pesa zilizosalia  halikusikizwa na kwa sababu ya  kukosa utu na kutojali kwa wahudumu katika hospitali  ile ,walimpa tembe ya kutoa mimba na wakamshauri  kwenda nyumbani .

‘ Niliambiwa niimeze usiku kasha nilale,alafu dawa itafanya kazi na  mabakai ya mtoto yangevuja yenyewe’ anasema Millicent .

Milly  alifiriki ingekuwa kazi rahisi lakini  alichojionea sasa ni  kumbukumbu ambazo zinamkwaza na kumtoa machozi kila uchao . Baada ya kumeza dawa aliyopewa ili kuitoa mimba ,mabakai ya mtoto yalianza kutoka kama damu .  Chumba chake cha kulala kilijaa damu na vipandd vya kijusi . Harufu iliyotanda katika chumba hicho ilikuwa ya  kumfanya mtu atapike lakini Milly kwa sababu ya usiri hakutaka usaidizi . Mamake alikuwa katika chumba tofauti na hakujua binti yake alikuwa akifanya nini kwa sababu alimuambua kwamba hatoenda kazi kwa  wiki moja kwa sababu ana maumivu .Mama  mtu hakujua binti yake alikuwa akiteleza mauaji mle ndani !

Uchungu , hofu ,harufu , damu na vipande vilivyochanika vya  kiumbe  vilitapakaa katika kitanda na chumba kizima cha Milly .hakujua la kufanya kwani alikuwa akivuja kama mrefeji .Alijikokota na kuifikia simu yake ili kumwita  binamu yake wa rika lake  ambaye boma lao linapakana na kwa akina Milly . Binamu  yake alipofika katika kile chumba alipatwa na butwaa asijue kilichokuwa kikifanyika .

‘ Nilimuambia anivute vyote  vilivyokuwa vikinitoka’aliniangalia kwa hofu asijue kilichokuwa kikifanyika ,hapo ndipo nilipojua kwamba nimefanya kosa kubwa ‘ anasema Milly

Binamu yake alipopata ufahamu wa kisa hakufanya alivyomtaka Milly .mara moja alikimbia kumwita mama Milicent na kumueleza kilichokuwa kikifanyika .Mama mtu alizarin alipoyaona yote mle chumbani . Milly alimdanganya binamu yake kwamba mimba ili ilitoka yenyewe lakini alisahau kutupa kipakiti cha tembe ya kuavya mimba aliyoimeza . Mbio mbio teksi iliitwa ili apelekwe hospitalini.Hospitali ya kwanza  waliokimbilia iliwakataa.Madaktari walisema  Milly alikuwaakiavya mimba na kamwe  hawangemhudumia . Hospitali ya pili waliokimbilia ni ile ya Kangemi ambako alipewa ile tembe ya kutoa mimba .Walipofika ,wahudumu hawakuonyesha majuto yoyote na walionekana kughadhabishwa kwamba mbona hakuwa na pesa za kumalizia utaratibu wote wa kuavya mimba hiyo .Walimchukua na kumepeleka wadi ili kumsafisha na kutamatisha ukatili ambao waliuanza kwa kumpa Milly tembe ile .

‘Kila siku nikiona mtoto mchanga,nakumbwa na  hisia zenye mkizano-najuta kwa kumuua mtoto wangu na pia naogopa tena kupata uja uzito .Sina uhakika iwapo mola ataniadhibu kwa kuninyima mtoto kwa ajili ya nilichofanya’ anasema Milly akidondokwa chozi la majuto.