Kwenda Uko!Nani amesema Stivo Simple Boy hapendwi na wakenya?

OCTO.jfif
OCTO.jfif

NA NICKSON TOSI

Msanii wa nyimbo za kufoka  Henry Ohanga almaarufu kama Octopizzo amejitokeza na kudai kuwa hapendezwi na vile wakenya wanachukia nyimbo za Stivo Simple Boy.

Katika mahojiano na mtandao fulani wa humu nchini, Octopizzo alisema kuwa Simple Boy ni msanii anayefanya kazi kwa bidii na hivyo ni sharti wakenya kuheshimu nyimbo zake kama ule wa Mihadarati na Tuheshimu ndoa.

Kama njia ya kudhihirisha hamaki yake kwa wakenya, Octopizzo alisema kuwa kuna baadhi ya wakenya ambao hawawezi andika hata sentensi tatu kwenye mtandao wa Twitter lakini ndio wa kwanza kuzikashifu nyimbo za Stivo simple Boy.

"Napenda hiyo ya mihadarati hizo zingine bado ndio nataka kuctach up sijaziskia sana cz one ni ngoma ilitoka kitambo na nafurahi sana ilifika time wase wanamwangalia kama msanii kitu nachukia ni wase wengine wanamchukulia kama comedian na ni msanii mserious anapenda art yake, anaifanya na roho yake yote hiyo ndio kitu watu hawajui. Hata akiongea unaeza tell anafanya hii kitu na roho yake yote but watu wengine wanaichukulia kama joke. Mi hukasirika mse haezi andika mistari tatu kwa twitter anachekelea msanii amedu ngoma na akashoot video, ka unajua unaeza criticize andika mistari tupatane kwa uwanja" alisema Octopizzo.

Akiulizwa iwapo amedinda kufanya mziki na Papa Jones ,Octo alisema kuwa Ppa Jones hajawahi mfikia na nia ya kutaka washirikiane ili kutoa wimbo.

“Mimi hajai nipigia simu the last time tulipatana nlikua nalaunch Wakiritho kwa Trace. Tukapiga mastory tukaongea. Halafu most of the time si hupatana time ya kazi. Hajai nipiga simu akasema Buda uko area gani nlikua nataka tuchapiane ama kuna mabeats kadhaa nlikua nataka usikize. Hivyo ndio mi hufanya nikita collabo na mtu Fulani. Nampigia simu hata kama sina number yake namtafuta. Hajai nipigia simu na akona number yangu na ya manager wangu"alisema Octopizzo.

“First naeza mwambia Ohanga si rapper Ohanga ni CEO. Rapper ni Octopizzo so ameitisha the wrong person collabo. Akitaka Collabo aongee na Octopizzo, Mr Ohanga ni CEO kumfikia ni ngumu, rada chafu”aliongeza Octopizzo.

 Octo aliwataka watu kukoma kumfananisha na Khaligraph kwa sababu wote hao wanafanya miziki tofauti na wako katika vitengo tofauti katika sanaa ya muziki.

Kuhusiana na usemi wake kuhusu Kuhalalishwa kwa bangi nchini,Octo alisema kuwa mmea huo unastahili kuahalalishwa kwa sababu unatoa tiba kwa baadhi ya magonjwa.