PATANISHO: mume wangu hajawahi ni nunulia nguo tangu anioe

Katika kitengo cha patanisho mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Kisii ambaye  anaitwa Emma Kwamboka,29, alituma ujumbe ili apanishwe na mume wake Kamau,38, ambaye walikosana baada ya kuwa katika ndoa kwa miaka miwili na nusu.

Emma alisema kuwa wana watoto wawili na walikosana kwa ajili mumewe hakutimiza matakwa yake ambayo alikuwa amemehahidi.

"Mume wangu ni mpaka rangi, tulikuwa tumesikizana aninunulie vitu vya wanawake, alipolipwa alirudi nyumbani akiwa amelewa chakari

Hapo nilipomuuliza alinichapa kichapo cha mbwa mpaka majirani wakakuja kunisaidia." Alieleza Kwamboka.

Mumewe alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi sitaki kurudiana na mwanamke huyo hii ni kwa sababu ni mlevi sana anapoenda kulewa uwa anakuja anavunja kila kitu kwa nyumba na hata uwa anauza vitu nyumbani anaenda kulewa

Kuna wakati alikuwa anaachia mwanawe wa kwanza mtoto wake wa pili akiwa na miezi tatu anaenda kulewa chakari.

Kwa kweli mimi sitaki kurudiana na yeye kwa maana nimevumilia ya kutosha, na nataka kumwambia aende akatafute mtu wa kabila lake amuoe." Alisema Kamau.

Kwambika hakukimya tu mbali alijitetea na kusema,

"Yeye mwenyewe ndiye amenifunza kunywa pombe alikuwa anakuja nayo nyumbani nikiwa mjamzito na kuniambia nikunywe

Jambo ambalo tunakosania kila mara ni kwa sababu, hajawahi ni nunulia nguo tangu anioe ata nguo moja hajawahi mimi nataka kumwambia kuwa nampenda na hasiwahi kuja kunitafuta kwa maana amesema hanitaki." Kwamboka Aliongea.

Kwa uondo zaidi tembelea mtandao wa kijamii wa Youtube.