Coronavirus:Kisa kingine charipotiwa Kericho na mwanamme kutengwa

Mwanamme mwenye umri wa miaka 47  ametengwa katika wadi maalum huko Londiani katika kaunti ya kericho kwa kushukiwakauwa na virusi vya corona .

Mwamanamme huyo alipelekwa katika hospitali hiyo na mkewe baada ya kulalamikia maumivu ya viungo vya  mwili na kukohoa ,daalili ambazo madaktari wanasema ni za virusi vya Corona .Ni mhubiri anayeripotiwa  kuwasili kericho maajuzi kutoka mkutano huko Mombasa na kisa hicho kiliripotiwa sikau ya jumamosi lakini kikafichuliwakwa umma siku ya jumatatu .

Gavana wa Kericho Paul Chepkwony na  afaisa mkuu anayesimamia huduma za matibabu David Ekuwam  wamethibitisha kisa hicho.Mke wa mwanamme huyo ameshauriwa kusalia nyumbani  ili kufahamu hali yake .