Mnapayuka nini?wacheni kulaumu rais Kenyatta! asema Vera Sidika

NA NICKSON TOSI

Mfanyabiashara maarufu kutoka Kenya Vera Sidika sasa amejitokeza na kuwashtumu wakenya kwa kile anasema haikuwa makosa ya raids Kenyatta kuruhusu ndege ya kutoka Uchina kutua nchini.

Kwa mujibu wa Vera ,kupigwa marufuku ndege kutoka eneo moja si suluhisho kwa kuzuiya virusi vya Corona bali taifa lilifaa lipige marufuku kuwasili nchini kwa ndege kutoka mataifa ya kigeni,hatua ambayo labda ingesaidia kuzuiya mkurupuko wa virusi hivyo nchini.

“sasa watu wengi wamekuwa wakimlaumu Rais Kenyatta kwa kuruhusu ndege kutoka uchina kutua nchini,nimekuwa nikijadili na watu ambao wamekuwa wakionelea eti ndege hiyo ndiyo iliyochangia Corona kutua nchini,maoni ambayo ni upuzi kwangu,kwa kweli iwapo kuna kitu ambacho kilistahili kufanyika ni kupigwa marufuku kwa ndege zote kutua nchini.Maoni ya Vera Sidika

Yanajiri haya baada ya Vera kutuma ujumbe wa jumbe alizokuwa ametumiwa na rafikiye zilizokuwa zinadai kuwa iwapo ndege hiyo ingekatazwa kutua nchini basi tungekuwepo na mgogoro wa kidiplomasia baina ya Kenya Uchina.

Vera aidha alimfahamisha jama huyo kuwa Corana haikuwasilishwa na ndege wala kutoka katika taifa la Uchina na kuongeza kuwa iwapo hata serikali ingezuiya kutua nchini kwa ndege hiyo basi mtu kutoka Uchina angesafiri kutoka Uchina hadi Uingereza na kutua nchini akiwa na virusi hivyo.

Kwa sasa ndege za Uchina zimezuiya kutua Kenya lakini hiyo iliyotoka Uingereza ilikubaliwa na kuwabeba waliokuwa wameathiriwa na virusi hivyo,huwezi kabiliana na tatizo hilo kwa sasa,na watu waache kulaumu serikali.alidai Vera