Watu 3 zaidi wapatikana na virusi vya Corona nchini na kufikisha idadi ya walioathirika kuwa 31

mwangangi
mwangangi
NA NICKSON TOSI

Wizara ya afya kupitia kwa afisa mkuu msimamizi Mercy Mwangangi  imethibitisha kuwa taifa la Kenya limesajili visa vitatu zaidi vya Coronavirus na kufanya idadi ya watu walioathirika na virusi hivyo kufikia watu 31.

Wizara hiyo pia imesema  watu 906 wanaosemekana kukaribiana na waathiriwa wa virusi hivyo  wanasakwa na serikali huku 123 wakiwa wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kufanyiwa vipimo.

Watu 18 nao wamelazwa katika hospitali ya Mbagathi wakisubiri kufanyiwa vipimo na madaktari.

Kaunti ambazo zimeripoti visa hivyo  vya Corona kulingana na wizara hiyo ni; Nairobi, Kilifi, Kwale, Mombasa na Kajiado.

Watatu hao waliopatikana na virusi hivyo wote ni wakenya wawili kutoka kaunti ya Kilifi na mmoja kutoka kaunti ya Nairobi.

Watu zaidi ya 2000 waliofika nchini Jumatatu wameambiwa wajitenga ili kuzuiya kusambaa kwa virusi hivyo kwa watu wengine.

Mhariri: Davis Ojiambo