Corona Movies/Series: Filamu zenye maudhui yanayofanana na zimwi la Coronavirus unazoweza kutazama (Part 1)

Muda huu ambao watu wametakiwa kuwa nyumbani   ili kuzuia kuambukizwa au kusambaza virusi vya Corona ,watu wengi wana muda wa kutosha kufanya shughuli zote na kusalia na muda wa ziada unaoweza kutumiwa kujipa angalau burudani .

Kutazama Runinga na vipindi vya kwaida kunaweza kuchosha lakini filamu  za msururu na  baadhi ya filamu kubwa tajika zinaweza kukusadia kupoteza muda na usijue hata giza limeingia vipi haraka . Kwa sababu ulimwengu kwa sasa unakabiliana na virusi vya Corona ,sehemu ya kwanza tazama filamu hizi ambazo zinahusiana na milipuko ya maradhi.Baadhi yazo zitakufanya ufikiri walioziunda walijua virusi vya Corona vitakuja kuangamiza ulimwengu wakati mmoja .

 

  1. Contagion (2011)

Iwapo  wewe ni mpenda filamu ,Contagion sio  movie ngeni kwako na  tangu kuchipuka kwa virusi vya corona ,watu wengi wamekuwa wakiitafuta filamu hii ili kuitazama tena kwa sababu maudhui yake ni kama zimwi la corona linaloangamiza ulimwengu wa sasa . Filamu hii ya mwaka wa 2011 inawashirikisha wazito katika uigizaji Matt Damon na Jude Law  na inasimulia jinsi watalaam wa afya ,serikali za mataifa ,maafisa wa  serikali  na watu wa kawaida wanapojipata pabaya katikati ya mlipuko wa maradhi yasiojulikana huku shirika la CDC likitafuta tiba . Hakuna filamu inayozungumzia mlipuko wa maradhi ambayo inafaanisha taswira yake kama hali ambayo ulimwengu upo sasa . Filamu hiyo ya muda wa saa moja na dakika 46 ,itakupa  mtazamo wa hofu na hali ilivyo kote duniani kwa ajili ya janga la sasa la corona .

  1. Kingdom Season 1&2(2019)

Filamu hii ya msururu  ya Korea kusini imetazamwa sana wakati wa janga hili la virusi vya corona hasa barani Asia .  Series hiyo yenye  Sehemu mbili na jumla ya episodes 12  inasimulia  mchipuko wa maradhi yasiojulikana katika ufalme ambao  kiongozi wake anaugua na mwanamfalme  ndiye  pekee mwenye uwezo wa kuwaokoa watu katika Ufalme huo . Baadaye mfalme anapoaga dunia ,anafufuka  kisha ugonjwa usiojuliakana unaanza kuwaangamiza watu .Mwanamfalme anasalia na kazi ngumu na kibarua kikubwa cha kukabiliana na adui mpya  ili kuwaokoa watu wengi . Netflix tayari imethibitisha kwamba  Sehemu ya Tatu ya Kingdom itatolewa ingawa haijajulikana itakuwa tayari lini .

 3.Containment Season 1 (2016)

 Series hii ya mwaka wa 2016 ilitolewa sehemu moja pekee   lakini utajipata na kasi ya moyo kujaribu kujifikiria kujipata katika hali ya waathiriwa ndani ya maigizo haya. Mtunzi wa series hii Julie Plec  anasimulia jinsi maradhi yasiojulikana yanavyozuk Atlanta  ,Amerika  na kulazimisha Jiji zima kubwa kuwekwa chini ya Lockdown na kuwaacha waliomo ndani kupigaia maisha yao . Hakuna kinachotisha kama kufikiria kuhusu kuachwa katika sehemu moja na watu walioambukizwa maradhi yasiojulikana waliwageukiwa wale ambao hawajaambukizwa ili kuwaangamiza.Iwapo  unahofu ya kupata ndoto za kuogofya au jinamizi ,basi epuka kuitazama hii . Msururu mzima una episodes 13

4.Outbreak 1995

 Outbreak  ni filamu ya  muda wa saa 2 na dakika 7 inayosimulia jinsi ugonjwa unaosambazwa hewani   unavyolipuka Marekani na kuwaangamiza watu .  kazi ya afisa wa Jeshi  kanali Sam Daniels ni kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo  katika mji mmoja mdogo  ambao unafaaa kutengwa na  maeneo mengine . Daniels pia amepewa jukumu la kuhakikisha kwa ikulu ya Whitehouse haichukua hatua ‘kali’ kwa sababu ya hofu ili kuwaangamiza wote wanaoishi katika mji huo mdogo.Sounds familiar?

 Wakati  virusi hivyo vinapoendelea kusababisha maafa na mahangaiko  katika mji huo wa Carlifornia , madaktari wa kijeshi wanapambana kutafuta  dawa . Katika  Outbreak  inadaiwa virusi hivyo vilitoka kwa nyani mmoja aliyeingizwa Amerika kutoka Afrika.Laiti wangelisema China ..

5.Cordon (2014)

 Series hii yenye sehemu mbili  iliandikwa na  , kuelekezwa na  Tim Mielants  na kutayarishwa na  . Inazungumzia mlipuko wa virusi katika jiji la Antwerp na hatua ya serikali kuamua kuwafungia watu walioambukizwa katika sehemu moja kutumia ukuta mkubwa .

 Series hii ilipeperushwa Uingereza  katik BBC Four  mwaka wa 2015 ,na hakuna aliyejua kwamba miaka mitano baadaye ,mlipuko wa virusi kama hivi utazifanya nchi kama Italia kutamani kujenga ukuta kuwazuia walioambukizwa wasitangamane na wasio na virusi  vya corona . Series ya Containment  Ilitayarishwa kutoka muigo wa  Cordon kwa ajili ya  Kituo cha CW  Network na kupeperushwa Marekani mwaka wa 2016.

 6.Helix (2014/2015)

 Helix iliyotayarishwa mwaka wa 2014 na 2015 ,inawaangazia watafiti wanaofika eneo la Arctic ili kuchunguza chimbuko  la viruysi hatari  ambavyo vimelipuka katika kituo cha kimataifa cha utafiti katika eneo hilo lililo mbali na binadamu . Helix ina seasons Mbili na  jumla ya episodes  26 zitakazokuweka katika kila taswira ya jinsi mambo yanavyoweza kubadilika na kuwa mabaya wakati huu tunapoendelea kupambana na virusi vya Corona . Watafiti wanaotegemewa kutafuta tiba ,wanajipata katika hali mbaya wakati baadhi yao wanapoambukizwa virusi hivyo hatari . Helix ,itakupa hofu kisha ukirejeshee matumaini  na ikupe  fikra ya kinachoweza kuwa mwisho wa  ulimwengu .

 Utafiti,Tathmini na Uandishi   umefanywa na Yusuf Juma ,kutegemea kumbi za filamu mtandaoni na usaidizi wa maelezo ya ziada  na MJ Mohammed.Haki  miliki za picha zilizotumiwa  ni za wenye filamu.