Habari za Hivi Punde! Prince Charles apona Corona

charles
charles
NA NICKSON TOSI

Mwanamfalme Charles  mmoja wa viongozi wakuu wa kifalme Uingereza ameruhusiwa kutoka kwenye karantini rasmi na madaktari wake baada ya hali yake ya afya kuimarika pakubwa.

Charles mwenye umri wa miaka 71, alipatikana na virusi hivyo wiki jana na alikuwa amewekwa chini ya uangalizi katika makao yake yaliyoko Scotland kwa takriban siku 7.

Serikali ya Uingereza imeweka sheria ya watu kujiweka kwenye karantini kwa takriban siku 7, swala ambalo limemfanya mkewe Charles, Camilla, kujitenga na familia yake ikiwa ni njia tu ya kutathmini iwapo aliambukizwa virusi hivyo na mumewe.

Viongozi wakuu wa Uingereza wamekuwa wakipatikana na virusi hivyo siku za hivi maajuzi akiwemo waziri mkuu Boris Johnson na waziri wa afya Matt Hancock.

Kufikia sasa, Uingereza imerekodi vifo 1228 vilivyotokana na  Corona na wataalam wanahofia kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka siku za hivi karibuni.