Yvonne alikuwa akitoa maoni yake lakini wengi katika KOT hawakuwa tayari kuheshimu maoani yake na wakageuza patashika zima kuwa shambulizi la ndani na masuala ya kibinafsi huku wengine hata wakipiga mashimo katika ndoa yake na taaluma yake katika uanahabari .
Baada ya msururu wa mashambulizi hayo kuna ‘Jenerali’ mmoja ambaye aliibuka kwa ujasiri kuja kumtetea Okwara . Miguna Miguna kupitia twitter aliwashauri wanatwitter kuhehsimu demokrasia na uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake bila kumvamia kuhusu masuala ya kibinafsi lakini ushauri huo uliingia katika sikio lililozibwa .
Miguna aliwashauri wanaomkosoa Okwara kufanya hivyo kupitia njia ya maoni yao na ushahidi bali sio kubinafsisha suala hilo kwa kuanza kumpaka tope kuhusu maisha yake ya ndoa na wengine hata kuanza kukosoa maumbile yake .