Mtoto wa Diana! Bahati afanyiwa kejeli baada ya video yake akidensi na mkewe Diana Marua

Msanii Bahati amejua sana kujiwekea mtego na wiki hii amekula vijembe kwa njia ya kikatili mtandaoni .

Msanii huyo amefanyiwa masimango na kejeli baada ya  rapa  Khaligraph Jones kutoa wimbo wake ambao ulimtaja Bahati kama ‘Mtoto wa Diana’ .

Bahati alijaribu kuteka   mawimbi ya wimbo huo kwa kutoa picha iliyomuonyesha akiwa amebebwa na Diana na hivyo kweli alifaulu kupepezea chini kejeli ambazo zingemfuata. Lakini alipoamua kuvalia kama mwanamke na kushiriki shindano la Tik tok na Diana, Bahati alifungua bomba kubwa la kufanyiwa mzaha na  huenda hakutarajia mlipuko wa hisia kama hizo

Haya hapa baadhi ya maoni ya wanamitandao

namelesskenya Woiiii…bhangi hiyo haikuwa imekauka vizuri… ‍♂️‍♂️

jalangoo Umechizi

djjoemfalme Bro nilishakushow. Turudi EMB buda….Ama nikustaki kwa @akotheekenya. Hii energy turudishe kwa kazi

akotheekenya Nitahama hii Kenya haki

clemmo25 Corona itatuonyesha mengi!!

gabu_bugubugu Umama umekuingia sasa. Happy mothersday

mzaziwillytuva Mwezi wa mfungo umeanza  Tuzidishe #Maombi

dansonko Vitu kama hizi ndio zimefanya tuongezewe 21 days zingine aki!

wesleytheedj Uko sawa buda?

weezdom254 Unakaa tule tudem hukula fare

yycomedian Halafu unapata tu kuna mwanaume wa Cameroon atanyonga na hii video bila kujua ni ndume…

felistarbrigita   mtoto wa dayana sasa utakuwa mama dayana

munju_ree bahati umeanza umama

goldshine___ Vipe tena bahat ushakuwa dulla makabila