Kivuko cha Mauti! Watu wanne waangamia baada ya boti kupinduka mto Kerio

Boat
Boat

NA NICKSON TOSI

Watu wanne wanaripotiwa kuwa wameaga dunia baada ya boti waliyokuwa wanatumia kuvukia mto Kerio kupinduka.

Kamanda wa polisi Samuel Ndanyi amesema miongoni mwao ni watoto wawili, mwanamume na mwanamke walikuwa miongoni mwa watu 18 waliokuwa wanavuka mto huo wakitumia boti hiyo Jumanne .

Ndanyi amesema kuwa miili hiyo ilipatikana baada ya wenyeji, maafisa wa KWS na polisi wa utawala kuendesha msako wa kutafuta miili hiyo usiku mzima.

Mwakilishi wa wadi ya Kerio Delta Peter Ekaru amesema eneo halijawai kushuhudia tukio kama hilo.

Watu wengine 14 waliokolewa wamepelekwa katika hospitali ya Kerio.