Kijana wa miaka 17 atafutwa na polisi baada ya kutoroka kwenye karantini licha ya kuonyesha dalili za corona

unnamed (26)
unnamed (26)
Maafisa wa usalama katika kaunti ya Embu wameanzisha msako wa kumtafuta kijana wa miaka 17 ambaye ametoroka eneo alilokuwa anazuiliwa baada ya kuonyesha dalili za corona.Mkuu wa afya kaunti hiyo Rosalyn Kaugi amesema kijana huyo alitokea katika kaunti ya Nairobi ambayo ilikuwa imefungwa kutokana na visa vya kuongezeka kwa Corona.

Kulingana polisi kijana huyo alikuwa anazuiliwa katika hospitali kuu ya Embu level 5.

Wamesema kuwa kijana huyo alikuwa anaishi katika kijiji cha Karurina ,Embu Magharibi na kuwafanya wakaazi wa eneo hilo kumripoti katika asasi kuu.

Kaugi amesema kuwa iwapo kijana huyo alikuwa na virusi hivyo hatari huenda akawaambukiza wengine kutoka upande huo.

“Once he is traced and tested, we will take the next measures depending on the test results," Kaugi amesema.

Ameongezea kuwa sasa uongozi wa kaunti hiyo utasalia ange ili kujiandaa kivyovyotye vile kukabiliana na virusi hivyo iwapo vitaripotiwa kaunti hiyo