Maafisa kutoka DCI watia watu 3 mbaroni wakiwa wamebeba vilipuzi

EZvjTCIWsAIAIJV.jfif
EZvjTCIWsAIAIJV.jfif
Makachero kutoka idara ya upelelezi nchini DCI wamewatia watu watatu waliokuwa wanasafirisha vilipuzi  eneo la Maili Tisa katika barabara kuu ya Namanga Nairobi.

Watatu hao ni Moses Koite, Patrick Ng'ang'a na Sadic Harabe ambaye ni raia wa kigeni wa miaka 26.

Kulingana na DCI, watatu hao walikuwa wanatumia gari aina ya Toyota Noah lenye nambari ya usajili KBM 880U  ambapo vifurushi takriban 100 vilipatikana vikiwa vimefungwa kwa makundi 17 tofauti.

“The suspects are in lawful custody pending further police action. Further investigations on the matter ongoing, ”imesema DCI .