'Walikuwa wa kushangaza,' Size 8 awasifu Bien na Bensoul kwa kufanya haya

Msanii wa nyimbo za injili Size 8 alitoa albamu yake mpya ili kusherehekea miaka saba ya wokovu. Akiwa kwenye mahojiano alisema kibao chake cha kwanza katika albamu hiyo cha 'yahweh' ni cha kushukuru.

Kibao hicho kilikuwa kimeandikwa na wsanii wa bendi ya sauti sol, Bien na Bensoul.

"Albamu yangu ya neema ina vibao saba vya kusherehekea miaka saba tangu niokoke, hii ni kumshukuru Mungu kwa yote ambayo amenitendea katika safari yangu ya wokovu."Alieleza Size 8.

Msanii huyo alisea kuwa Bien na Bensoul walikuwa wa kushangaza walipokuwa wakiandika kibao hicho;

"AS A RESULT OF ALL GOD HAS DONE FOR ME THIS FAR. OUT OF GRATITUDE TOWARDS HIS DOING IN MY LIFE, WE WENT OUT TOGETHER [AND] DID AN ALBUM TITLED NEEMA TU

THE MAIN MESSAGE IS TO APPRECIATE GOD FOR THE JOURNEY SINCE I WAS YOUNG. THE SONG WAS WRITTEN BY BIEN AND BENSOUL AND THEY WERE JUST TOO AMAZING." Alizungumza.

Size 8 alisema kuwa kibao hicho kiko karibu na moyo wake na huwa anakiskiza kila wakati.

“I CRY EVERY TIME I LISTEN TO IT. GOD HAS BROUGHT ME FROM FAR. THERE ARE SO MANY THINGS HE HAS DONE YET I’M NOT THE BEST

MY BABIES ARE BOTH MIRACLES. ENDORSEMENTS JUST KEEP FOLLOWING ME. I LOVE MY GOD SO MUCH

I WAS SICK TO THE EXTENT I COULD NOT COME OUT OF BED BUT GOD STILL SAVED ME.”

Kibao Yahweh kimepokelewa vyema na mashabiki na kinaenea sana kwenye mitandao ya kijamii ya youtube.