Joho ni rafiki! Asema Alikiba

Ali Kiba amesifia urafiki baina yake na kiongozi wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho akisema ni mengi wamefunzana kwa muda huo wote.

Mara nyingi msanii huyo kutokea Tanzania amekuwa akionekana na gavana Joho wakiwa katika mitaa tofauti ya Mombasa.

Akizungumza na mwanahabari Willis Raburu, Kiba alisema kuwa Joho amemfaidi pakubwa katika maisha yake jambo ambalo analishukuru kila mara.

“We are good and we talk, he is one of my favourite friends that encourage me in life. he is very wise and teaches me about business. Joho likes people to be successful ,” alisema Alikiba

Wakati wa harusi yake mwaka 2018, Joho alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa wanahudhuria harusi hiyo.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, Alikiba na Joho walionekana wakiwa pamoja wakielekea kutathmini shughuli ya upigaji kura katika vituo tofauti vya eneo hilo.

Miongoni mwa wasanii wengine kutokea Tanzania ambao wana uhusiano mwema na Joho ni kama Ommy Dimpoz, Nandy,