Wakati wa kikao na wanahabari afisa mmoja mkuu katika wizara hiyo Dr Pacifica Onyancha amesema akina mama wanafaa kuwaacha wanao kutunzwa na mtu mwingine pindi wanapomaliza kuwanyonyesha .
Pia amewakumbusha wazazi walo na watoto walip chini ya umri wa miaka miwili kutowavalisha maski kwani hatua hiyo inaweza kuhatarisha maisha ya wanao .
" watoto ni viumbe dhaifu sana … maski inaweza kuhatarisha maisha yao kwani inapunguza kiasi cha hewa wanayopumua’ Onyancha amesema
Onyancha pia amesema watoto walio chini ya umri wa miaka 5 hawafai kuvalia maski wakiwa ndani ya gari kwani wanaweza kulala na kisha kukosa pumzi .Kenya jumanne ilirekodi visa vipya 133 vya virusi vya corona na kufikisha jumla ya visa 3,860.
Visa hivyo vilipatikana baada ya sampuli 3,255 kupimwa katika saa 24 zilizotangulia .waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema hadi kufikia sasa Kenya imepima sampuli 121,926.