'Today marks 5 months since she rested,' Joyce Gituro azungumzia kumpoteza dada yake baada ya kutoka Milele Fm

Aliyekuwa mtangazaji wa Milele Joyce Gituro kwa mara ya kwanza amezungumzia ama ukipenda amefunguka kuhusu maisha yake baada ya kutoka katika stesheni hiyo.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram Gituro ambaye anafanya kazi sasa katika stesheni ya Radiojambo alisema kuwa Milele ilikuwa inamlipa mshahara mzuri bali aliamua kuondoka kwa ajili ya sababu zake kibinafsi.

Baada ya miezi saba kupita alimpoteza dada yake na kisha kumaliza tena miezi kumi na moja bila kazi ilhali Mungu alikuwa naye kwa hayo yote.

Leo,22,Juni waliokuwa wafanyakazi wenzangu wamefutwa kazi na mediamax na wengi watazidi kufutwa katika siku za usoni

Nataka kushauri mtu na kumwambia kuwa asimame kidete kwa maana Mungu anaweza, atatembea nawe katika nchi kavu anajua mahitaji yako maishani mwako na kusudi lake kuwa maishan mwako litatimia

Katika kitabu cha Isaya 41:10 neno la Mungu linasema;10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu  ." Gituro Aliandika.