Uncle Willy,Tuko na wewe! Omanga amwambia Ruto

Seneta mteule Millicent Omanga ameshangaza wengi baada ya kuonekana akiwa kwa hafla iliyokuwa inaongozwa na naibu rais William Ruto kwake nyumbani na hata kusikika akisema kuwa wapo pamoja .

Katika mkutano huo,Ruto alikuwa anaungana na wabunge ,MCAs na viongozi wa vijana ili kutoa ufadhili wa vyombo vya kuwasaidia kujisimamia kimaisha.

"Uncle Willy, hadi huko bunge tuko na wewe," Omanga alimwambia Ruto.

Usemi wa Omanga unajiri wiki kadhaa baada ya kusema kuwa anashirikiana na rais Uhuru Kenyatta ili kufanikisha ajenda zake kwa taifa.

Omanga ni miongoni mwa maseneta wa chama tawala cha Jubilee amboa walitishiwa kupoteza nafasi zao baada ya kuonekana wakijiinigza kwa kampeni za mapema hivi kukaidi amri ya rais.