Matiang’I aliyekuwa akizungumza katika taasisi ya KICD katika mkutano na viongozi kutoka Murang’a amesema amekuwa akipokea simu kutoka kwa viongozi wa kidini wanaohofia kwamba huenda michezo hiyo ya kubashiri ikirejea tena na kuwateka vijana baada ya sheria kulegezwa ili kuruhusu kampuni hizo ziendelee na oparesheni yazo nchini
“ Hatutabadilisha sheria hizo kwa sababu tunataka unadhifu enya .michezo ya kamari nusura iiharibu Kenya .wahalifu na watu wanatakatisha fedha walikuwa wakinawiri na wengine walikuwa wmetoka mashariki mwa Uropa.walikuwa wakifanya mambo ambao hawangeyafanya katika mataifa yao’ amesema Matiang’i
Waziri huyo amesema kwamba serikali inaheshimu uamuzi wa bunge kuhusu suala hilo huku akiongeza kwamba hakuna leseni iliyotolewa kwa kampuni ya michezo ya kubashiri mwaka huu wa kifedha kwa sababu wanangoja idhini ya wizara ya afya kwa ajili ya janga la corona .
Dr Matiang’I Pia amesema serikali hivi karibuni itaanzisha awamu ya pili ya msako dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya katika kaunti za Murang’a na Kiambu .