Rais Uhuru Kenyatta afungua shughuli za usafiri katika majimbo yaliyokuwa yamefungwa

EcPJA4OXkAABVK8.jfif
EcPJA4OXkAABVK8.jfif
Katika hotuba yake kwa taifa ,kiongozi wa taifa ameamuru kurejelewa kwa shughuli za usafiri ndani na nje ya kaunti zilizokuwa zimefungwa za Nairobi, Mombasa na Mandera ili kufufua uchumi wa taifa.

Amesema iwapo ongezeko la virusi vya corona vitaendelea kuongezeka nchini ,hatachelea kuchukua hatua za haraka.

Amesema agizo la kufungua miji hiyo mitatu inatimia saa 4 asubuhi.

Wakati uo huo Uhuru amesema maagizo ya kafyu yataendelea kote nchini kuanzia saa 9 usiku hadi saa 4 asubuhi kwa siku 30.

Amewataka wakenya kuendelea kuwa ange katika maeneo ya kufanyia kazi kutokana na ongezeko la virusi ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa nchini.

Ameongezea kuwa ni sharti wakenya kuendelea kufuata maagizo ya wizara ya afya ili kusaidia serikali katika vita vya kukabiliana na virusi vya corona.

"By reopening Nairobi, Mombasa, and Mandera, we must be aware that we will all be more at risk. We must exercise cautious optimism. Avoid reckless abandon." -Uhuru Kenyatta.

Maeneo ya kuabudu nchini pia yameruhusiwa kurejelewa shughuli za kawaida japo kwa kuzingatia vigezo na masharti ambayo yametolewa na serikali.

Vikao kama madrassas na Sunday schools katika makanisa nchini vimepigwa marufuku na rais Kenyatta .

Aidha watu 100 pekee ndio watakao ruhusiwa kuhudhuria misa mbali mbali katika maeneo ya kuabudu nchini.

Watu kati ya miaka 58 na ambao wanashida mbali mbali za kiafya wamepigwa marufuku nkuhudhuria vikao vya kanisa .

Magari ya uchuguzi wa umma yamepigwa marufuku kusafiri nje na ndani ya kaunti ambazo zilikuwa zimefungwa .

Ndege za kimataifa zimeruhusiwa kuanza safari zake za ndani kuanzia Agosti Mosi mwaka huu 2020.

Ndege za ndani zimeruhusiwa kuendelea na shughuli zake kuanzia Jumatano hii tarehe 15  kwa kufwata vigezo .

Vile vile marufuku ya watu kukusanyika katika maeneo ya harusi ,mikutano ya kisiasa na mikutano mingine imepigwa marufuku kwa siku 30 zaidi.

Kiongozi wa taifa aidha amewataka washikadau katika sekta ya elimu nchini kufanya vikao na kubuni namna shughuli za masomo zitakavyorejelewa nchini.

 For us, to remain open and revive the economy, all Kenyans must come together. For us to do this, we must change our National mind set, chart the future that is ahead of us;President Kenyatta:

Rais Kenyatta ameelezea masikitiko yake makubwa kutokana na ongezeko la visa vya mimba za mapema miongoni mwa wasichana wa umri mdogo akiwataka wananchi na mashirika mbali mbali kuripoti visa vya unyanyasaji.

Ametaka shirika la kuangazia maslahi ya watoto nchini kutoa taarifa kamili ya watu wanaowadunga mimba wasichana nchini ili kuchukuliwa hatua za kisheria,