Seneta wa Baringo amwakilisha rais Kenyatta kwa hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa Malawi

EcOl650XgAEBGP4.jfif
EcOl650XgAEBGP4.jfif
Seneta wa Baringo Gideon Moi na katibu katika wizara  ya maswala ya kigen Ababu Namwamba wamemwakilisha rais Kenyatta katika hafla ya kuabishwa kwa rais Mteule wa taifa la Malawi Lazarus Chakwera.

Hafla hiyo inayofanyika hii leo imeratibiwa kuhudhuriwa na wageni 100.

Kama njia ya kuanza majukumu yake mapya, Chakwera alitupilia mbali maadhimisho ya kaudhimisha siku ya Uhuru wa taifa hilo akisema pesa ambazo zingetumika kuandaa hafla hiyo zitasaidia kukabiliana na virusi vya corona.

Kufikia sasa taifa hilo limesajili visa 1,498 vya maambukizi ya corona.

Hafla hiyo itahudhuriwa na watu 10,000 kutoka kwa idadi ya watu 20,000 kama ilivyokuwa imeratibiwa kufanyika .