Hii ni baada ya kampuni ya Telkom Kenya kuingia katika makubaliano na kampuni inayomiliki google Alphabet kwa kiasi kisichojulikana cha fedha kuzitumia baluni maalum kuwezesha mawasiliano ya intenet duniani.
Akizungumza katika kituo cha Radat Huko Baringo wakati wa uzinduzi huo kupitia WhatsApp video, rais pia aliwahutubia waliohudhuria hafla hiyo na kuwataka waitumie vyema huduma hiyo na miundo misingi mingine iliyoboreshwa ya mawasiliano kudumisha shughuli za kiuchumi kuleta kipato.
"Sasa mna internet yenye kasi zaidi na mtandao wa kutegemewa. Mnaweza sasa mkauza asali yenu kwa ulimwengu mzima, itumieni fursa hii vizuri’ rais amesema.
Waziri Wa ICT Joe Mucheru ametaja uzinduzi huo kama wa kihistoria akiongeza kwamba Kenya inazidi kuwa mstari wa mbele duniani kuhusu masuala ya teknolojia .