Wawakilishi wadi wamechukua pesa za kuwalipa wafanyakazi wa afya-Waiguru

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru amesema kuwa hatapitisha bajeti ya mwaka wa 2020/2021 baada ya kubadilishwa na wanachama wa bunge.

Waiguru ambaye amekuwa na ugomvi na wawakilishi wadi alisema kuwa  mabadiliko hayo si halali.

"The County Executive presented the Financial Year 2020/2021 proposed budget to the County Assembly for approval, the Assembly submitted a completely new budget with a variation of over 30 percent per vote, going against the requirement of Regulation 37(1) of the Public Finance (County Government) Regulations 2015 which limits the assembly variations to 1 percent of the ceilings." Waiguru Alisema.

Gavana huyo aliwaambia wawakilishi wadi hao waweze kufikiria tena kitendo chao na kuweka mahitaji ya wananchi mbele wala si yao.

Alidai kuwa wawakilishi wadi hao walichukua, millioni 300 zilizopangiwa kuwalipa wafanyakazi wa afya na kusema kuwa ni za kujenga afisi za wadi.

Pia alisema kuwa MCAs hao walichukua millioni 20 za kuwalipa wafanyakazi wa kusafisha vifaa vya afya, kulingana na Waiguru bunge hilo pia lilinyakua millioni 14.6 za kuweka ambulensi mafuta, okseji