Hali hiyo imeleta hali ya mkanganyiko katika mrengo wake na kwenye uongozi wa ANC huku Mudavadi akisema yuko tayari kumrithi rais Uhuru Kenyatta.
Kiongozi huyo wa ANC amezidisha shughuli zake za kisiasa lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kambi yake bado ina mgawanyiko na haijafanya uamuzi thabiti kuhusu uchaguzi huo.
Kwa upande mmoja kuna washauri wake wanaomataka ajiunge na kambi ya naibu wa Rais Willian Ruto, kwa upande mwingine baadhi ya washirika wake wanamtaka amkaribie rais Uhuru Kenyatta ili aweze kumtaja kama mrithi wake na pia kupiga jeki juhudi zake za kutaka kuwa rais.
Mwaka wa 2002, Mudavadi alikaidi wimbi la upinzani Narc na kumuunga mkono Uhuru Kenyatta na chama cha Kanu walioshindwa katika uchaguzi huo licha ya kuungwa mkono na rais Daniel Moi.
Aliyekuwa waziri Franklin Bett ameliambia gazeti la The Star kwamba ingawaje Mudavadi ni mwanasiasa stadi, hajaweza kujitokeza kwa ukakamavu kupigania nafasi yake kuchukua usukani katika siasa.
" Wimbi la 2022 linaonekana kuwaegemea wale wanaounga mkono mwafaka wa BBI’ amesema Bett .
Hata hivyo naibu kiongozi wa chama cha ANC Ayub Savula amesema Mudavdi anasalia mgombeaji thabiti wa kuchukua nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa 2022.