Asilimia 96 ya wanawake katika sekta ya nyumba wamepitia dhuluma

Takriban asilimia 90 ya wanawake katika sekta ya mali isiyohamishika au real estate, wamepitia dhulma za kijinsia wakiwa kazini. Utafiti wa dhulma za kijinsia katika sekta hio unaonyesha kuwa asilimia 92 ya waliohojiwa wameshawahi kupitia dhulma hizo huku asilimia 82 wakishuhudia zikitekelezwa.

Dhulma hizo zinajumuisha zinazotolewa kwa maneno, na unyanyasaji wa kingono.

Visa vya dhulma dhidi ya watoto vinaweza kupungua humu nchini, iwapo tutakubali ulezi wa kijamii. Mwanaharakati wa haki za watoto Betty Adera anasema ingawaje jamii inahitaji kuwajibika kila mara wanaposhuku kuna dhulma dhidi ya watoto, inahuzunisha kuwa ubinafsi umekithiri.

Kwingineko, wakulima huko Dundori, katika kaunti ya Nakuru sasa watapokea mbolea ya bure kutoka kwa serikali. Haya yanajiri baada ya bunge la kaunti kupitisha hoja ya kutambua juhudi zao.

Mwakilishi wa wadi wa Dundori Michael Machembu anasema usalama wa chakula hautaafikiwa iwapo wakulima hawatatambuliwa na kupewa mbolea au pembejeo zingine za kupiga jeki uzalishaji chakula.

Mbali na hayo, Tana River jana ilikuwa kaunti ya hivi karibuni kuripoti kisa cha Covid-19. Hii inaifanya idadi ya kaunti zilizo na maambukizi ya corona kufikia 44 kwa sasa. Pia tulirekodi idadi kubwa zaidi ya visa vya maambukizi jana ikiwa ni visa 688.