Katibu wa kudumu wa mashauri ya kigeni Macharia Kamau alipatikana na virusi hivyo wiki jana na akumkabidhi katibu wa diplomasia balozi Tom Amollo majukumu yake .
Lakini Macharia alijutia kwamba mpango wa serikaliwa kuwatafuta watu waliotangamana na waliopatikana na ugonjwa huo umefeli ,hakuna matibabu na utunzi wa walipatikana na ugonjwa huo na pia kampuni za bima zimekataa kugharamia matibabu ya wagonjwa hao .
“ kwa mabilioni yote yaliyotengwa kw akampeini hii ni jambo la kufadhaisha kwamba hakuna hata mkakati wa kuhakikisha kwamba waliopta ugonjwa huo wanapata huduma za matibabu au hata kuweza kuwatafuta watu wengine waliotangamana na wagonjwa’ Macharia alisema katika kundi moja la WhatsApp la maafisa wakuu wa serikali
Maoni yake hayo huenda yakalipua kutoridhika kwa namba ambayo wizara ya afya inashughulikia janga hilo huku pakiwa na hofu kwamba huenda visa vya corona vikalemaza mfumo wa huduma za matibabu nchini .
Maafisa kadhaa wakuu wa serikali wamekuwa wakipambana pia na virusi hivyo baada ya kuambukizwa wakiwemo mawaziri wawili .
Macharia amesema pindi tu alipopimwa na kupatikana na virusi vya corona aliwaarifu watu wote aliokutana nao lakini alishangaa kwamba hakuna aliyekua amejulishwa hilo na serikali kumaanisha kwamba mpango huoulifeli kitambo .
Macharia amesema alikuwa na daalili kama za ugonjwa wa malaria na kizungungu lakini bado hajakwnda hospitalini .
NHIF wiki jana ilitangaza kwamba iatagharamia huduma za utunzi kwa wagonjwa wa Covid kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali zilizoidhinishwa na wizara ya Afya .