Mwanasosholaiti Huddah Mnroe yupo Dubai na akiwa huko amezungumza kuhusu kuhusu kukamatwa kwa mwanablogu Edgar Obare ambaye amekuwa akifichua mahusiano ya wanasiasa na mahusiano yao ya kimapenzi.
Amesema kukamatwa kwa Obare ni ishara ya jinsi watu wanaoeneza uvumi wanafaa kuadhibiwa kwa kuvunja ndoa za watu ilhali masuala ya kibinafasi ya watu yanafaa kusalia siri .
Huddah alisema ;
Watu kama hao wanafaa kukamatwa ,kupigwa na mikono yao kuvunjwa! Ili wasiweze tena kuchapisha tena chochote katika maisha yao
Kero lake hilo lilielekezwa dhidi ya Edgar Obare akimuambia awafichue watu ambao humpa habari hizo za siri .
Huddah aliyafichua hayo wakati wa maswali na majibu alipowauliza wanachokosa kumhusu
Huddah hajasazwa siku za hapoo nyuma na wanablogu kuhusu kazi ambayo yeye hufanya na pia alieleza kwamba anachukia sana uvumi na masengenyo