Angalau vijana,200,wajawazito wapatwa na virusi vya ukimwi Murang'a

5b23a5a6ac0563167cb02c67
5b23a5a6ac0563167cb02c67
Kulingana na mtendaji mkuu wa afya Joseph Mbai angalau vijana 200 wajawazito katika kaunti ya Murang'a wamepatikana na virusi vya ukimwi.

Katika data iliochukuliwa katika hospitali kuu ya Murang'a level 5 vijana 4,000 wamo wajawazito katika umri wao mdogo.

Pia kulingana na Mbai nambari ilirekodiwa kwa wasichana waliona virusi vya ukimwi hiko juu kuliko hali ya kawaida, Murang'a ina watu 16,000 wanaoishi na virusi vya ukimwi huku, 4000 wakiwa ni vijana wa jinsia zote mbili.

Kaunti ya Murang'a imeanzisha kampeni ya kuwapima vijana virusi hivyo na hata kuwashauri endapo watapatikana na virusi hivyo.

"Mpango huu utatusaidia kupata data za ndani ambazo zinawakilisha hali sahihi katika upimaji wa virusi hivyo." Alizungumza Mbai.

Vijana watakao patikana na virusi hivyo watawekwa katika ratiba ya matibabu huku wakipewa dawa za ukimwi (ARV's)ili kuzuia mtoto kuambukizwa.