‘ Nilipoteza uzani kupindukia nikijaribu kupata mimba’ Wema Sepetu

Wema
Wema
Aliyekuwa Miss Tanzania Wema Sepetu amesema  mojawapo ya sababu zilizomfanya kuacha kujaribu kupata mimba ni kwa sababu alipatwa na maambukizi .

Wema alilazimika kwenda India kwa matibabu kwani iwapo angeendelea kutaka kupata mtoto basi huenda angejipata pia na kansa .

Akizungumza   katika mahojiano na Clouds FM  Wema amesema ;

 ‘ sikufanyiwa upasuaji wa kupungu tumbo langu kama wanavyosema watu . sababu yangu kwenda india ilikuwa kupata ushauri na matibabu  ya kuweza kupata mimba .

  niliporejea nilishauriwa kupunguza uzani  kwani hatua hiyo ingezidisha uwezo wangu kumapat mimba  kwa sababu ilikuwa na mafuta mengi karibu nza mfuko wa uzazi

 Wema  ameongeza kwamba baadhi ya tembe alizokuwa akimeza zilikuwa zikimfanya  kuzidisha uzani .  Tembe hizo pia zilivuruga homoni zake na kufanya kuwa vigumu kwake kupata watoto .

 ‘ watu wanajua jinsi nilivyojaribu kupata mtoto na  furaha yangu itakamilika nitakapopata mtoto .

 niliongeza uzani katika jaribio langu la kupata mimba  na nimetumia dawa nyingi  ambazo zilikuwa na athari za pembeni .