‘ Walisema baba ya mtoto wangu ni MCA na Watchman’ Awinja atoa sababu za kumficha mtoto wake

Vicke
Vicke
Jacky Vike aka Awinja  ni  mama anayempenda sana mtoto wake  Mosi.  Muigizaji huyo  hata hivyo hajawahi kuonyesha sura ya mwanawe  katika  mitandao ya  kijamii  na katika mahojiano na  MC Jesse alisema sababu moja ya kutofanya hivyo ni  vijembe vya mitandaoni ambavyo watu hupenda kufanya kuhusu maisha ya watu na kuwashambulia .

 ‘…WATU WANAANZA KUMWAMBIA NI MU UGLY. THEN I’M LOOKING AT IT VILE HATA YEYE HATAJUA BUT SIDHANI KAMA NAWEZA KUWA NA HIYO PATIENCE YA KUTOLERATE SUCH COZ I’LL INSULT YOU SO I’M AVOIDING THAT.

Awinja  alisimulia jinsi  watu walivyomhuisisha na msururu wa wanaume wakati alipokuwa mja mzito

NILIWEKELEWA WATU KAMA EIGHT MPAKA MCA WA HUKO USHAGO KWETU HATA SIJAWAHI JUA ANAEXIST MPAKA NIKAMWONEA HURUMA. MPAKA KULIKUWA NA WATCHMAN.

Muigizaji  mwenzake  Wilbroda alichangia  kuhusu hilo akisema ;

‘ mitandao ya kijamii ni kama ushetani .. imetusaidia sana lakini kuna mabaya mengi ndani yake  .nahisi kuanza kumueka mtoto wake katika mitandao ya kijamii akiwa mdogo sio jambo zuri . lazima nipate idhini yake .

https://www.instagram.com/p/CAAf3WgHhrA/

Aliongeza

 hebu fikiria mtu akisema kwamba mtoto wako ana sura mbaya? wakati mwingine hapo awali mtu aliwahi kusema hivyo baada ya picha tuliochukua katika hafla moja kusambazwa .

…”HUYU MTOTO ANAKAAJE, WAPI BABAKE..”.  tangia hapo nilijiambia sitawahi kuiweka picha yake mtandaoni hadi awe mkubwa  na ajiamulie mwenyewe .

Wilbroda pia alisema anapendelea kumficha mtoto wake kutoka macho ya mitandao ya kijamii

 Naweza  kupigana vita vyangu  mwenyewe ,maoni ambayo watu hutoa … watu wana hila  sio kila mtu atahisi mema  ama kwa njia sawa kukuhusu .