Subiri urogwe! Zari Hassan amwambia Mama Dangote

Kwa Muda sasa Sandra yaani mama Dangote amekuwa akimposti mjukuu wake  Latiffah Dangote (Princess Tiffah) kwenye mitandao ya kijamii.

Katika moja wapo ya posti zake Zari Hassan alitoa maoni huku akimwambia mama ya staa wa bongo aweze kusubiri arogwe.

"Umezidi,subiri urogwe." Aliandika Zari.

Maoni yake hayakupokelewa vyema na mashabiki wake Hamisa Mobetto ambapo walisema kuwa alikuwa ana mkejeli na kumkosoa Hamisa.

Wanamitandao walidai kuwa Zari alimaanisha kuwa Hamisa anaweza roga Mama Dangote ili hasimpende mjukuu wake vile anavyompenda.

Itasalia kwenye kumbukumbu za wanamitandao na watu wengi kuwa Diamond alijitokeza na kusema kuwa kuna wakati Hamisa alikuwa anataka kumroga.