Seneti kwa mara ya nane yashindwa kukwamua utata wa mfumo wa ugavi wa mapato

mgao
mgao

Seneti siku ya Jumanne kwa mara ya nane ilishindwa kupata suluhu kwa utata unaozingira mswada wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti.

Huku ikionekana kuwa maseneta walikuwa tayari wanaelekea kupiga kura, kiongozi wa wachache James Orengo aliingilia kati na kubadili mkondo wa mjadala.

Soma habari zaidi;

Orengo alisema seneti haiwezi kupigia mswada huo kura na ilhali palikuwepo mabadiliko yaliyokuwa wamependekezwa na kamati ya seneti ya Fedha na Bajeti.

Mabadiliko hayo yanapendekezwa na seneta maalum Petronilla Were, Kimani Wamatangi (Kiambu), Ledama Olekina (Narok) na James Orengo wa Siaya.

Were anataka pendekezo la Tume ya ugavi wa mapato kukubaliwa kama mfumo wa tatu wa ugavi mapato.

Hata hivyo, seneta huyo anapendekeza kuwa mfumo wa sasa uendelee kutumika na kwamba mfumo wa tume ya CRA uanze kutumika wakati kiasi za mgao wa usawazishaji utakapopandishwa hadi shilingi bilioni 348 kutoka kiasi cha sasa cha bilioni 316.5.

Soma habari zaidi;

Hoja ya Orengo ilimlazimu Spika kuahirisha upigaji kura ili kuruhusu mjadala kuhusu mapendekezo hayo mapya.

Maseneta sasa watakuwa na kikao siku ya Alhamisi kujaribu kukwamua swala hilo hili.