Siogopi 'system au deep State' Ruto afoka

Naibu rais William Ruto kwa mara nyingine tena amesema kamba haogopi kile wapinzani wake wanaita 'deep state' au 'system' ambayo anasema juhudi zake ni kusambaratisha azma yake ya urais.

Ruto alisema kwamba ikiwa agekuwa muoga, yeye na rais Uhuru Kenyatta hawangeunda serikali ya sasa.

Soma habari zaidi;

“Kama rais Uhuru na mimi tungekuwa waoga, hatungeunda serikali chini ya JP. Tulitishwa na madai mengi, ikiwemo kesi zetu za ICC wakati huo, ambazo zilikuwa uongo,” Ruto alisema.

Naibu rais alizungumza siku ya Jumanne nyumbani kwake mtaani Karen Nairobi alipokuwa mwenyeji wa viongozi wa jamii kutoka eneo bunge la Kajiado Kusini, wakiongozwa na mbunge Katoo Ole Metito na Seneta Mary Seneta.

Matamshi ya Ruto pia yanajiri baada ya naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe kuwaambia wakenya kujiandaa kwa uongozi wa Raila mwaka 2022.

Murathe alikuwa amesema kwamba Raila amepigania nchi hii sana na anastahili kuzawadiwa.

Ruto alisema kwamba matokeo ya uchaguzi wa 2022 yataamuliwa na wapiga kura, na kupuuzilia mbali ushawishi wa 'deep state au system'.

"Eti kuna watu fulani wameketi mahali ambao watafanya uamuzi.”

Soma habari zaidi;

Ruto aliongeza kuwa wapiga kura watakuwa na usemi wa mwisho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Naibu rais alitowa wito kwa viongozi waliochaguliwa kusimama wima dhidi ya nguvu zozote zinazolenga kuhujumu ahadi zao za uchaguzi.